Kujiuzulu kwa Iran Kutoka JCPOA Na Matokeo yake Duniani.
Baada ya mauaji ya Jenerali wa Irani Qasem Soleimani na Amerika na mfululizo wa matukio uliofuatia, hali ya hivi karibuni ni kwamba Irani imetishia kwamba inaweza kuachana na Mkataba wa Kupunguza Ongezeko la Nyuklia, NPT (Nuclear Non-Proliferation) ikiwa Umoja wa Ulaya ulipeleka suala la nyuklia ya Irani kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UNSC). Hii ni maadhara kubwa zaidi baada ya kuuawa kwa Jenerali Soleimani, kwani athari zake zinaweza kuwa mbaya sana kwa bara nzima na kwa serikali za mataifa YA NPT. Tishio la kujiondoa kutoka NPT linakuja baada ya uamuzi ulioripotiwa wa serikali ya Irani kwamba haitafuata tena masharti ya Mpango wa Utendaji Kamili wa Pamoja (JCPOA), maarufu kama makubaliano ya nyuklia ya Iran.
Wito wa Iran wa kujiondoa kutoka NPT ni majibu ya kuanzishwa kwa Mbinu ya Kutatua Mizozo (DRM), kifungu kilichowekwa katika makubaliano ya nyuklia, na kundi la nchi tatu za Ulaya Uingereza, Ufaransa na Ujerumani, ambazo zilikuwa sehemu ya mpango huo. Ukweli kwamba Amerika iliripotiwa kushinikiza nchi za Ulaya kuchukua njia hii inaonyesha kwamba kuendelea kwa shinikizo kama hilo kwa Wazungu kunaweza kusababisha kujiondoa kabisa kwa Irani kutoka JCPOA.
Kuanzishwa kwa DRM na baadaye kupeleka suala la nyuklia la Irani kwa UNSC kunaweza kusababisha kurudishwa kwa vikwazo vya UNSC juu ya Iran. Iran tayari imekuwa ikiteseka kutokana na athari za kiuchumi za vikwazo vya nchi moja vilivyowekwa na Amerika, na iliyosababisha mvutano mkubwa ndani ya nchi. Vizuizi vingine zaidi vya kimataifa vinaweza kuashiria mvutano zaidi ya ndani, na kusababisha tishio kali kwa utawala wa Kiislamu, na hatimaye uwezekano wa kulipiza kisasi kwa maandamano vikali kupinga hayo na serikali ya Irani kunaweza tokea.
Mzozo uliopo kati ya Irani na Amerika unaweza kuonekana kama matokeo ya kujiondoa kutoka kwa JCPOA na Rais wa Amerika, Donald Trump mnamo Mei 8, 2018, licha ya udhibitisho wa mara kwa mara wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) kwamba Iran ilikuwa ikitimiza ahadi zake zilizowekwa katika mpango huo. Kwa kweli, Iran ilikuwa imengoja kwa mwaka mmoja baada ya kujiondoa kwa Amerika kwa matumaini kwamba mataifa ya Ulaya yatapata suluhisho, kukashindikana, Iran ikatangaza mnamo Mei 8, 2019, kwamba ilikuwa ikikomesha kujitoa kwake kwa JCPOA.
Kusudi la msingi la JCPOA lilikuwa kudhibiti kasi ya utajirikaji wa Irani na urani, kujiondoa kwa Iran kutoka kwa aina hiyo kunamaanisha kasi kubwa ya utajirikaji na Iran. Jambo lingine muhimu la JCPOA lilikuwa uwazi wa mpango wa nyuklia wa Irani na kwa hivyo kujiondoa kwa Iran katika mpango huu pia kutamaanisha kwamba mataifa mengine hayataweza kujua asili halisi na maendeleo katika mpango wa nyuklia wa Irani.
Hofu kama hizo zinazohusiana na mpango wa nyuklia wa Irani zinaweza kusababisha mataifa mengine, haswa, Saudi Arabia mpinzani wa kikanda wa Irani, kufuata njio hio, na kusababisha mchuano wa nyuklia katika kanda ya Mashariki ya Kati. Hii inaweza pia kuchochea mataifa mengine ynayopinga mpango wa nyuklia wa Irani kama vile Marekani na Israeli kushambulia kijeshi mitambo ya nyuklia ya Irani, na kusababisha hali ya sasa ya migogoro kuongezeka kuwa vita. Inaweza pia kusisitizwa katika muktadha huu kwamba kwa sababu ya nafasi yake kama hifadhi tajiri ya hydrocarbon, vita katika eneo la Ghuba ya Uajemi vinaweza kuwa na athari mbaya kwenye uchumi wa ulimwengu.
Waziri wa Mambo ya nje wa Iran Mohammad Javad Zarif alikuwa New Delhi wiki iliyopita. Alifanya mazungumzo ya kina na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi na Waziri wa Mambo ya nje Dkt S Jaishankar. New Delhi ilionyesha hamu yake ya amani katika Ghuba ya Uajemi.
Taarifa ya hivi karibuni ya Mkuu wa Ofisi ya Rais wa Iran Mahmoud Vaezi, akihimiza Iran na Saudi Arabia kufanya kazi pamoja, ni ya kutia moyo. Nchi za Ghuba ya Uajemi zinapaswa kufanya kazi kwa pamoja kurejesha na kudumisha usalama katika eneo hilo. Hii ni muhimu sana kwa amani na utulivu wa kikanda, na ili kupunguza kuenea kwa nguvu ya nyuklia, nchi hizo mbili za mkoa zinapaswa kupata njia za kidiplomasia za kutatua tofauti zao.
Comments
Post a Comment