Nepali Yahirisha Majadiliano juu ya Marekebisho ya Katiba.

India na Nepali wameunganishwa na mpaka wa ardhi wa kilomita 1750 unaojumuisha majimbo matano ya India yakiwa, Sikkim, West Bengal, Bihar, Uttar Pradesh na Uttarakhand. Wingi wa mpaka huu uliimarishwa na makubaliano ya Sugauli yaliyosainiwa mwaka wa 1816 kati ya kampuni ya East India na mahakama ya kifalme ya Nepali. Ilinakilisha mto wa Kali (Mahakali) kama ukomo wa magharibi ya Nepali. Hiyo ni kwamba eneo la Nepali inapatikana tu Mashariki mwa Kali.




Nepali hivi karibuni walizindua ramani mpya ya eneo lake wakidai karibu eneo la ukubwa wa kilomita 400 katika maeneo ya Kalapani, Limpiyadhura na Lipulekh, ambayo yalirekodiwa kama sehemu ya India na yaliyo Magharibi mwa Kali.




Kathmandu (jiji kuu la Nepali) yanadai kuwa maeneo haya yanapatikana mashariki mwa sehemu ya mto Kali yaani tributary ya Kali kwa lugha ya kiingereza na kwa hivyo ni sehemu ya Nepal. Hii ni hata baada ya ramani za miaka zaidi ya 150 zikiwemo ramani za Nepali pia zikiweka peupe kuwa sehemu kubwa ya mto Kali ni mto unaotoka Kalapani na hivyo inamaanisha maeneo haya ni magharibi wa Kali.




Maeneo ya jimbo la India la Uttarakhand karibu na mpaka wa Nepali na Uchina, yametumiwa tangu jadi na Watakatifu kutoka India wanaopitia Kailash Mansarovar Yatra. Ili kurahisisha safari ya watakatifu kuelekea Mlima Kailash na Mansarovar, India hivi karibuni walitamatisha ujenzi wa barabara kutoka Tawaghat hadi Lipulekh, inayojumuisha barabara inayotumiwa na Watakatifu. Barabara hii ilianzishwa mwezi wa Aprili mwaka huu wa 2020 na waziri wa ulinzi wa India.




Serikali ya Nepali ilijibu punde kwa kudai kuwa barabara hiyo ilipita ndani ya eneo la Nepal na wakatoa wito kwa Uhindi mapema mwezi wa May wakiwaarifu kuacha kufanya mashughuli yoyote ya ujenzi katika eneo hilo.




Siku chache baadaye, mnamo Mei 18, katibu la mawaziri la Nepali lilidhinisha ramani mpya iliyoongeza eneo la Nepali hadi Limpiyadhura. Ramani mpya ilizinduliwa tarehe 20 Mei na Waziri Mkuu wa Nepali K P Sharma Oli akitangaza katika bunge kuwa hili lilikuwa juhudi halisi la kurejesha ardhi ya Nepali.




Madai haya yasiyo na msingi yalipingwa vikali na India ikiomba Nepal kuacha kuchukua hatua kama haya na kuheshimu uhuru wa India na uadilifu wa maeneo. Zaidi ya hayo, matumaini yalionyeshwa kuwa uongozi wa Nepal utatengeneza mazingira bora kwa ajili ya mazungumzo ya kidiplomasia ili kutatua masuala ya mpaka. Nchi hizi mbili zinashirikishwa na maadili sawa za kitamaduni.




Uhusiano wa India na Nepal katika ngazi ya watu wa kawaida ni kati ya yaliyo ya kipekee na maalum na uhusiano za kuunganisha za dini na njia ya maisha. Uhusiano imara wa kiuchumi- India ndiye mwekezaji mkubwa wa nje katika Nepal na kwa ukubwa ndiye mbia wake wa biashara- unaonyesha zaidi ukaribu wa uhusiano wao.




Wakati ulimwengu, vilevile India na Nepali wakikabiliwa na janga la corona na wakati mgumu wa changamoto wa kiuchumu usio wa kawaida, nchi zote mbili wanafaa kufanya kazi kwa pamoja ili kutatua mateseko ya raia.




Suala kuu linalohusiana na ramani mpya ni kwamba linachora upya ramani ya Nepali ambayo imewekwa katika nembo ya kitaifa vile ilivyorekodiwa katika katiba ya nchi. Ili ramani mpya ipate kutambuliwa kisheria, marekebisho ya katiba inahitajika. Kuzingatiwa, mswada wa marekebisho ya katiba uliandikishwa kwenye bunge la Nepali na inafaa kuwa imechukuliwa kwa majadaliano tarehe 26 Mei. Marekebisho ya Katiba nchini Nepali inahitaji theluthi mbili ya uwingi kwenye bunge.




Nepali sasa imehirisha majadaliano katika bunge lake juu ya suala ya ramani mpya. Nchi zote mbili zimeonyesha ukomavu kwa kuheshimiana. Ni muhimu kuwa uhusiano wa nchi hizi mbili zitaimarishwa zaidi hadi ushirikiano wa karibu kati ya majirani hawa.

Comments

Popular posts from this blog

Mpango wa wazir mkuu wa India ,  unaoitwa Mann ki baat,  Maana yake ni maneno ya moyo, ambapo waziri mkuu wa India amehutubia watu wa taifa 

WAZIRI MKUU ANATOA WITO KWA AJILI YA KUWEKA MAPENZI YA TAIFA KWANZA

Kujiuzulu kwa Iran Kutoka JCPOA Na Matokeo yake Duniani.