Kuimarisha Uhusiano wa Biashara wa Uhindi na Amerika

Waziri Mkuu Narendra Modi amezitaka kampuni za Amerika kuwekeza nchini India, katika sekta mbali mbali ikiwemo miundombinu, uhandisi, ulinzi na utafiti wa anga. Alikuwa akihutubia Mkutano wa Mawazo ya India. Mkutano huu uliandaliwa na Baraza la Biashara la Amerika na India. Mada ya mkutano ilikuwa “Kujenga Maisha Bora ya Usoni mema”. Mkutano wa Mawazo ya India unakusudia kuvutia uwekezaji kutoka nje ya nchi kama ajenda ya urejeshaji baada ya COVID-19.




Waziri Mkuu Modi alielezea kuwa India ilipata dola bilioni 20 ya uwekezaji wa nje kwenye kipindi cha robo ya kwanza ya 2020-21. Alisema pia, hali ya Urahisi wa kufanya biashara ya India imeboreka. Matumaini ya uwekezaji yanaweza kuamua zaidi maboresho katika makadirio ya biashara kuu ya India. India imefikia rekodi kubwa katika uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni (FDI). Mabadiliko katika uwekezaji wa kigeni kutokakwa nyanja za FII hadi FDI ni hali inayokubalika kwani FDI ni uwekezaji thabiti kuliko Nyanja za uwekezaji wa kigeni. FII ni “pesa moto” na inaweza kusababisha ongezeko wa fedha za uwekezaji za kigeni kulingana na kiwango cha riba. Pesa moto daima huitikia viwango vya juu vya riba.




Waziri Mkuu alisema kuwa “kuongezeka kwa India kunamaanisha kuongezeka kwa fursa za kibiashara na taifa ambalo unaweza kuamini, kuongezeka kwa uingiliaji wa kimataifa na kuongezeka kwa uwazi, kuongezeka kwa ushindani wako na upatikanaji wa soko ambalo linatoa viwango bora. Na kuongezeka kwa mapato yako kwenye uwekezaji kwasababu ya upatikanaji wa rasilimali ya watu wenye ujuzi.” Alisema pia uwezekano wa uwekezaji katika teknolojia za juu za 5G, uchanganuzi mkubwa wa data, hesabu ya kompyuta, blockchain na mtandao wa vitu.




Bwana Modi alisema kuwa India na Amerika ni demokrasia mbili dhabiti, na kwa hivyo ni marafiki asili. Ushirikiano wa Amerika na Uhindi unachukua jukumu kubwa katika kusaidia ulimwengu kurudi haraka katika janga la covid19.




Wakati wa janga hili, uimara wa uchumi wa dunia unaweza kupatikana kikamilifu na kwa urahisi kupitia uwezo wa kiuchumi wa nyumbani. Waziri Mkuu alisisitiza umuhimu wa India kujitegemea katika paradigm ya “Atmanirbhar Bharat”. Mchanganyiko wa biashara ya kimataifa na uimarishaji wa masoko ya kifedha ni viashiria vingine vya uvumilivu wa ulimwengu. baada ya janga Ukosefu wa sera unaweza kufanya maendeleo iwe polepole.




Chaguzi za uwekezaji katika sekta ya kilimo ni pamoja na FDI katika usindikaji wa chakula, mazao ya mimea na uvuvi. Katika uwekezaji wa sekta ya afya - sekta ya pharma - Uhindi na Amerika wanaunda uhusiano wenye nguvu wa biashara. Katika sekta ya nishati, India inajitokeza kama uchumi unaotegemea gesi. Kutakuwa na fursa kubwa za uwekezaji katika nishati safi. Eneo lingine ambalo linawezatoa fursa kwa uwekezaji wa biashara ya Amerika na Uhindi uko katika miundombinu ikiwa ni kujenga nyumba kwa mamilioni, au kujenga barabara, barabara kuu na bandari.




Safari za ndege za raia pia kumetambuliwa kama eneo muhimu la ukuaji mkubwa. Waziri Mkuu alitaja kwamba idadi ya abiria wa Hewa wanatarajiwa zaidi ya mara mbili ndani ya miaka 8 ijayo. Kampuni za juu za Ndege za kibinafsi za India zina mpango wa kuleta ndege mpya zaidi ya elfu katika muongo mmoja ujao. Katika sekta za ulinzi na anga India imerekebisha kiwango cha FDI hadi asilimia 74. Katika sekta ya bima, cap ya FDI ni asilimia 100. India imeanzisha bidhaa nyingi za bima ikiwa ni pamoja na Ayushman Bharat - mpango wa uhakikisho wa afya, Pradhan Mantri Fasal Bima Yojna, mpango wa bima ya mazao na Jan Suraksha na miradi mingine ya usalama wa kijamii. Bwana Modi alieleza, njia mpya za bima ni afya, kilimo, biashara na bima ya maisha. Takwimu zinaonyesha kuwa mapato ya FDI yalifikia rekodi kubwa nchini India. Hii ni ongezeko la asilimia 20 kutoka mwaka uliopita.




Katikati ya COVID-19, India imeendelea kuvutia uwekezaji wa nje. Jambo linalopaswa kukumbukwa ni kwamba pamoja na uwekezaji wa nje, kuna haja kubwa ya India ya kuimarisha juu ya uwekezaji wa ndani wa kampuni binafsi. Ushuhuda wa nguvu unaonyesha kuwa uwekezaji wa miundombinu ya umma ni uamuzi mkubwa unaovutia uwekezaji wa kibinafsi. Waziri Mkuu aliweka mkazo katika kuimarisha uwekezaji wa miundombinu. Kushughulikia vikwazo vya miundombinu, kuhakikisha ukweli wa sera na uratibu wa sera za uchumi ni muhimu sana kufanikisha hili. Ili kuhakikisha urejesho wa uchumi katika kipindi cha baada ya janga, uwekezaji katika sekta za msingi ni muhimu sana.

Comments

Popular posts from this blog

Mpango wa wazir mkuu wa India ,  unaoitwa Mann ki baat,  Maana yake ni maneno ya moyo, ambapo waziri mkuu wa India amehutubia watu wa taifa 

WAZIRI MKUU ANATOA WITO KWA AJILI YA KUWEKA MAPENZI YA TAIFA KWANZA

Kujiuzulu kwa Iran Kutoka JCPOA Na Matokeo yake Duniani.