Waziri Mkuu Ataka Makampuni Mapya Kuwa na Matarajio Makubwa.

Waziri Mkuu Narendra Modi alihutubia nchi kupitia mpango wake wa “Mann ki Baat” kupitia redio ya All India Radio. Katika toleo la 68 la Mann ki Baat, Waziri Mkuu alisema kuwa vijana walishiriki katika hafla ya Ubunifu wa aplikisheni ya ‘AatmaNirbhar Bharat’. Alibainisha kuwa karibu theluthi mbili ya washirika wa hafla hio walikuwa vijana kutoka miji yenye idadi ya watu wa katikati (miji ya daraja ya pili na tatu). Matuzo yamepewa aplikisheni karibu dazeni mbili katika vitengo tofauti, alisema. Aliwauliza wasikilizaji wa redio ya All India Radio kupata kujifahamisha na aplikisheni hizi na kuungana nazo.




Waziri Mkuu alitaja aplikisheni hizi kadhaa, zikiwemo aplikisheni ya Kutuki Kids learning, aplikisheni ya watoto; aplikisheni ya jukwaa ndogo la kublogi au kuandika majarida inayoitwa ku KOO ku; Chingari App ambayo inakuwa maarufu kati ya vijana; aplikisheni ya ‘Ask Sarkar’ ambayo hupata habari sahihi juu ya miradi ya serikali na aplikisheni ya Step Set Go- fitness nk.




Waziri Mkuu Modi alisema kuwa makampuni haya madogo ya leo yatabadilika na kuwa makampuni makubwa hapo mbeleni na kuweka alama ya India ulimwenguni, akiongeza kuwa mtu asisahau kwamba makampuni makubwa ambayo yapo ulimwenguni kwa sasa, yalikuwa pia makampuni madogo yanayoanza.




Bwana Modi aliwasihi wanafunzi na waalimu kuleta hadithi za mashujaa ambao hawajapata kusifiwa kwa majuhudi yao katika mapambano yetu ya uhuru. Waziri Mkuu alisema kuwa wakati mtu anafikiria juu ya mafanikio yake, kila wakati hukumbuka mwalimu. Alisema kuwa janga la COVID-19 limesababisha changamoto kwa waalimu, ambao wameigeuza kuwa fursa kwa kukumbatia kwa urahisi zana mpya na teknolojia, ambazo wamezipitisha kwa wanafunzi wao pia. Alionyesha imani kuwa waalimu watachukua jukumu muhimu katika kusambaza faida za sera ya taifa ya elimu kwa wanafunzi.




Akitaja kuwa nchi itakuwa ikisherehekea mwaka wake wa 75 wa uhuru mnamo 2022, Waziri Mkuu alisema ni muhimu kwa wanafunzi wa leo kuendelea kujifahamisha na mashujaa wa mapambano yetu ya uhuru. Hapo ndipo tu wanafunzi wanaweza kuelimishwa juu ya historia ya mapambano yetu ya uhuru.




Waziri Mkuu alipendekeza kuwa mada ya utafiti kwa wanafunzi inaweza kuwa kupata ikiwa kulikuwa na hafla zozote wakati wa harakati za kupigania uhuru katika wilaya wanamoishi. Kutumbelea mahali katika miji yao inayohusishwa na vita vya uhuru na wanafunzi kunaweza kupangwa pia. Wanafunzi wa shule zingine wanaweza pia kuamua kuandika shairi 75 na hadithi za maonyesho juu ya mashujaa wa harakati zetu za uhuru kuashiria miaka 75 ya uhuru wetu, alisema.




Waziri Mkuu alibaini kuwa juhudi hizi zitaleta; hadithi nyingi za mashujaa ambao hawakupata kutambuliwa ambao walitumikia nchi yetu kwa uda na uvumba. Na siku ya Walimu ambayo itazingatiwa mnamo Septemba 5, Waziri Mkuu Modi alitoa wito kwa walimu kuanza kujiandaa na kufanya kazi ya kujenga mazingira kwa ajili ya juhudi hizo.




Bwana Modi alibaini kuwa mwezi wa Septemba unaangaliwa kama ‘Poshan Maah’ (mwezi wa Lishe). Alisema kuwa taifa na lishe vinahusiana sana. Alikumbuka kauli mbiu - “Yatha Annam Tatha Manam” ambayo inamaanisha kuwa maendeleo ya akili yanahusiana moja kwa moja na ubora wa ulaji wetu wa chakula. Alisema kuwa lishe na lishe bora inachukua jukumu kubwa katika kusaidia watoto na wanafunzi kupata uwezo wao mzuri na kuonyesha ustadi wao. Alisisitiza kuwa ili watoto wapate lishe bora, mama yao anahitaji kupata lishe bora. Aliongeza kuwa lishe haimaanishi tu kula lakini pia kupata virutubisho muhimu kama chumvi, vitamini nk.




Waziri Mkuu alisema kuwa katika darasa, kama vile kuna Kinara wa Darasa, inapaswa kuwa na Kinara wa Lishe. Vivyo hivyo, kama kadi ya Ripoti, Kadi ya Lishe inapaswa pia kuletwa. Alifahamisha kuwa wakati wa Mwezi wa Lishe, jaribio la chakula na lishe pamoja na mashindano ya meme yataandaliwa kwenye mtandao wa My Gov. Aliwauliza wasikilizaji kushiriki kwenye mashindano na jaribio haya.




Akisisitiza kwamba India imejaa na utofauti wa chakula na vinywaji, Waziri Mkuu alisema ni muhimu sana kwa mujibu wa msimu wa eneo fulani, mpango wa lishe bora na utajiri wa lishe kuundwa na kujumuisha nafaka za vyakula vya eneo hilo, matunda na mboga.

Comments

Popular posts from this blog

Mpango wa wazir mkuu wa India ,  unaoitwa Mann ki baat,  Maana yake ni maneno ya moyo, ambapo waziri mkuu wa India amehutubia watu wa taifa 

WAZIRI MKUU ANATOA WITO KWA AJILI YA KUWEKA MAPENZI YA TAIFA KWANZA

Kujiuzulu kwa Iran Kutoka JCPOA Na Matokeo yake Duniani.