Waziri Mkuu Asema Mageuzi Ndiyo Njia Pekee ya Mbele.
Waziri Mkuu Narendra Modi alizungumzia juu ya umuhimu wa Sera ya Taifa ya Elimu (NEP) 2020 wakati wa kikao cha uzinduzi wa Mkutano wa Magavana. Rais wa India Bwana Ram Nath Kovind pia alihudhuria hafla hiyo.
Waziri Mkuu alisema, Sera mpya ya taifa ya Elimu (NEP) sio ya serikali moja bali ni ya nchi nzima, na inapaswa kutekelezwa vilivyo bila kujali serikali iliyoko madarakani.
Aliweka mkazo kwa mazungumzo mbali mbali nchini juu ya utekelezaji wa sera, Waziri Mkuu alisema kuwa ufahamisho kati ya wanafunzi, walimu na wazazi kuhusu NEP inapaswa kuwa kamili kama mashauriano ya wadau ambayo yalisababisha kutungwa kwa sera yenyewe. Ufunguo wa mafanikio ya NEP, alisema, uko katika ushiriki wa wadau.
Bwana Modi alisema, “Ni muhimu pia kwamba ufahamu wetu (kuhusu NEP na faida zake) inapaswa kuwa ya kina na pana kama mchakato wa mashauriano. Ni muhimu kujadili faida zote na kila sehemu ya waraka huu. Inaweza kutekelezwa mara tu mashaka na maswali yote katika akili za watu yatakaposhughulikiwa ”.
Tunaposoga kuelekea mabadiliko, ni kawaida kwa mashaka na maswali kuibuka kwenye akili za watu. Wazazi wanaweza kujiuliza ni vipi hatua ya kufuta mitiririko ya masomo itaathiri maisha ya baadaye ya mtoto wao. Walimu wanaweza kutaka kujua jinsi mtaala wa masomo kama hayo utakavyoundwa. Wadau wataweza kuwa na maswali juu ya upatikanaji wa rasilimali za kutosha kutimiza malengo ya NEP, Waziri Mkuu alitambua. Aliwaomba Magavana wote waliokuwepo kwenye mkutano huo kufanya mikutano ya video hadi Septemba 25 katika majimbo yao ili kuboresha uelewa wa sera kati ya wadau.
Waziri Mkuu alisifu mashauriano mbali mbali yaliyofanywa na Wizara ya Elimu katika hatua za kuandaa rasimu ya kukubalika kwa NEP nchini. Alifafanua zaidi vifungu vya NEP. Alisema kuwa mafunzo ya vitendo au mafunzo ya ufundi katika umri mdogo yatasaidia na kuwezesha kuifanya India atmanirbhar (kujitegemea).
Ili kuifanya India kujitegemea, ni muhimu kwa vijana wetu kuwa na ujuzi. Kuzoesha ujuzi katika umri mdogo na ufunzaji wa vitendo utawasaidia vijana kuwa na uwezo wa kuajiriwa na hii pia itaongeza sehemu yetu katika soko la ajira ulimwenguni, Bwana Modi alisema. “Sera mpya ya Kitaifa ya Elimu pia inazungumzia juu ya kukabiliana na mazoea ya wataalam kuhamia nchi za ng’ambo. Ikiwa vyuo vikuu bora zaidi ulimwenguni vitakuja nchini India basi wanafunzi hawatataka kusomea nje ya nchi. Pia, vyuo vikuu vyetu vitakuwa na uwezo zaidi wa kushindana na mahitaji ya kuingia kwenye vyuo vikuu vya nje” Waziri Mkuu alisema.
Bwana Modi alisema kuwa kadri tunavyojifunza na kuelewa mambo anuwai ya Sera mpya ya Kitaifa ya Elimu itakuwa wazi na rahisi kuitekeleza, na kukubalika. Alisema kuwa sera hii imebuniwa na kuumbwa kwa kipindi cha miaka mitatu hadi minne kabla ya hapo mchakato mkubwa wa kufikiria na utafiti vile vile maoni na rasilimali zilimwagiwa katika kupanga na kuweka vilivyo muundo wa sera ya sasa ya Elimu.
Waziri Mkuu alishughulikia ukweli kwamba kote nchini Sera ya Kitaifa ya Elimu ilikuwa ikizungumziwa, kujadiliwa, kutazamwa na kupitiwa ambayo itathibitisha kufikia utekelezaji mzuri na wenye mafanikio na vile vile kuwa na athari nzuri kwa malengo ya taifa ya kielimu.
Waziri Mkuu alisema, mageuzi ndiyo njia pekee ya kusonga mbele na yatafaidi sio tu kizazi ya sasa lakini pia ilikuwa vizazi vijavyo katika mtazamo na upeo wake. Alisema kuwa Sera ya Kitaifa ya Elimu ya India itakuwa nguzo mwanzilishi wa karne ya ishirini ya India na pia kuipeleka katika enzi mpya. Sera hiyo itahakikisha vijana wetu wako tayari kwa maisha ya usoni, aliongeza zaidi kuwa mageuzi ya haraka ya elimu yatawezesha vijana wetu kujifunza haraka na kwa njia inayojumuisha zaidi.
Sera ya Kitaifa ya Elimu inajumuisha na pia kunufaisha kila mtu katika upeo wake na haina upendeleo wowote. Waziri Mkuu alisema, mageuzi yaliyoletwa yanazingatia na kuongeza zaidi mahitaji ya nyakati zinazobadilika haraka na mienendo ya changamoto za kijamii, kisiasa na kiuchumi.
Comments
Post a Comment